20. Laumu imenivunja moyo,Nami ninaugua sana.Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna;Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.
21. Wakanipa uchungu kuwa chakula changu;Nami nilipokuwa na kiu wakaninywesha siki.
22. Meza yao mbele yao na iwe mtego;Naam, wakiwa salama na iwe tanzi.