3. Bali wenye haki hufurahi,Na kuushangilia uso wa Mungu,Naam, hupiga kelele kwa furaha.
4. Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake,Mtengenezeeni njia ya barabara,Apitaye majangwani kama mpanda farasi;Jina lake ni YAHU; shangilieni mbele zake.
5. Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane,Mungu katika kao lake takatifu.
6. Mungu huwakalisha wapweke nyumbani;Huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa;Bali wakaidi hukaa katika nchi kavu.
7. Ee Mungu, ulipotoka mbele ya watu wako,Ulipopita nyikani,
8. Nchi ilitetemekaNaam, mbingu zilidondoka usoni pa Mungu;Hata Sinai usoni pa Mungu; Mungu wa Israeli.
9. Ee Mungu, ulinyesha mvua ya neema;Urithi wako ulipochoka uliutia nguvu.
10. Kabila yako ilifanya kao lake huko;Ee Mungu, kwa wema wako uliwaruzuku walioonewa.
11. Bwana analitoa neno lake;Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa;
12. Wafalme wa majeshi wanakimbia, wanakimbia;Na mwanamke akaaye nyumbani agawa nyara.
13. Kwa nini kulala mazizini arukapo hua,Mbawa zake ziking’aa kama fedhaNa manyoya yake kama dhahabu?
14. Mwenyezi Mungu alipotawanya wafalme huko,Kulinyesha theluji katika Salmoni.