28. Ee Mungu, uziamuru nguvu zako;Ee Mungu, uwe hodari uliyetufanyia makuu.
29. Kwa ajili ya hekalu lako YerusalemuWafalme watakuletea hedaya.
30. Mkemee mnyama wa manyasini;Kundi la mafahali, na ndama za watu;Hata wanyenyekee na kuleta vipande vya fedha,Uwatawanye watu wapendao vita.
31. Masheki watakuja kutoka Misri,Kushi itamnyoshea Mungu mikono yake mara.
32. Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu,Msifuni Bwana kwa nyimbo.