Zab. 67:3-6 Swahili Union Version (SUV)

3. Watu na wakushukuru, Ee Mungu,Watu wote na wakushukuru.

4. Mataifa na washangilie,Naam, waimbe kwa furaha,Maana kwa haki utawahukumu watu,Na kuwaongoza mataifa walioko duniani.

5. Watu na wakushukuru, Ee Mungu,Watu wote na wakushukuru.

6. Nchi imetoa mazao yakeMUNGU, Mungu wetu, ametubariki.

Zab. 67