8. Na Wewe, BWANA, utawacheka,Utawadhihaki mataifa yote.
9. Ee nguvu zangu, nitakungoja Wewe,Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu
10. Mungu wa fadhili zangu atanitangulia,Mungu atanijalia kuwatazama adui zangu.
11. Usiwaue, watu wangu wasije wakasahau;Uwatawanye kwa uweza wako,Na kuwaangamiza, Ee Bwana, ngao yetu.