Zab. 58:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Ni kweli, enyi wakuu, mnanena haki?Enyi wanadamu, mnahukumu kwa adili?

2. Sivyo! Mioyoni mwenu mnatenda maovu;Katika nchi mnapima udhalimu wa mikono yenu.

3. Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao;Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.

4. Sumu yao, mfano wake ni sumu ya nyoka;Mfano wao ni fira kiziwi azibaye sikio lake.

5. Asiyeisikiliza sauti ya waganga,Ijapo wanafanya uganga kwa ustadi.

Zab. 58