1. Ni kweli, enyi wakuu, mnanena haki?Enyi wanadamu, mnahukumu kwa adili?
2. Sivyo! Mioyoni mwenu mnatenda maovu;Katika nchi mnapima udhalimu wa mikono yenu.
3. Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao;Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.
4. Sumu yao, mfano wake ni sumu ya nyoka;Mfano wao ni fira kiziwi azibaye sikio lake.