1. Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari?Wema wa Mungu upo sikuzote.
2. Ulimi wako watunga madhara,Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila
3. Umependa mabaya kuliko mema,Na uongo kuliko kusema kweli.
4. Umependa maneno yote ya kupoteza watu,Ewe ulimi wenye hila.
5. Lakini Mungu atakuharibu hata milele;Atakuondolea mbali;Atakunyakua hemani mwako;Atakung’oa katika nchi ya walio hai.
6. Nao wenye haki wataona;Wataingiwa na hofu na kumcheka;