2. Kwa kuwa BWANA Aliye juu, mwenye kuogofya,Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote.
3. Atawatiisha watu wa nchi chini yetu,Na mataifa chini ya miguu yetu.
4. Atatuchagulia urithi wetu,Fahari ya Yakobo ambaye alimpenda.
5. Mungu amepaa kwa kelele za shangwe,BWANA kwa sauti ya baragumu.
6. Mwimbieni Mungu, naam, imbeni;Mwimbieni mfalme wetu, naam, imbeni.
7. Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote,Imbeni kwa akili.