Zab. 44:7-17 Swahili Union Version (SUV)

7. Bali Wewe ndiwe uliyetuokoa na watesi wetu;Na watuchukiao umewaaibisha.

8. Tumejisifia Mungu mchana kutwa,Na jina lako tutalishukuru milele.

9. Lakini umetutupa, umetufedhehesha,Wala hutoki na majeshi yetu.

10. Waturudisha nyuma tukampa mtesi kisogo,Na watuchukiao wanajipatia mateka.

11. Umetutoa kama kondoo tuwe chakula,Na kututawanya kati ya mataifa.

12. Wawauza watu wako bila kupata mali,Wala hukupata faida kwa thamani yao.

13. Umetufanya kuwa lawama kwa jirani zetu,Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.

14. Umetufanya kuwa mithali kwa mataifa,Sababu ya kutikisa kichwa kwa watu wa nchi.

15. Mchana kutwa fedheha yangu i mbele yangu,Na haya ya uso wangu imenifunika,

16. Kwa sauti ya mwenye kulaumu na kukufuru,Kwa sababu ya adui na mjilipiza kisasi.

17. Haya yote yametupata, bali hatukukusahau,Wala hatukulihalifu agano lako.

Zab. 44