Zab. 40:7-11 Swahili Union Version (SUV)

7. Ndipo niliposema, Tazama nimekuja,(Katika gombo la chuo nimeandikiwa,)

8. Kuyafanya mapenzi yako,Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu;Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.

9. Nimehubiri habari za haki katika kusanyiko kubwa.Sikuizuia midomo yangu; Ee BWANA, unajua.

10. Sikusitiri haki yako moyoni mwangu;Nimetangaza uaminifu wako na wokovu wako.Sikuficha fadhili zako wala kweli yakoKatika kusanyiko kubwa.

11. Nawe, BWANA, usinizuilie rehema zako,Fadhili zako na kweli yako na zinihifadhi daima.

Zab. 40