Zab. 40:6-11 Swahili Union Version (SUV)

6. Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo,Masikio yangu umeyazibua,Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.

7. Ndipo niliposema, Tazama nimekuja,(Katika gombo la chuo nimeandikiwa,)

8. Kuyafanya mapenzi yako,Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu;Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.

9. Nimehubiri habari za haki katika kusanyiko kubwa.Sikuizuia midomo yangu; Ee BWANA, unajua.

10. Sikusitiri haki yako moyoni mwangu;Nimetangaza uaminifu wako na wokovu wako.Sikuficha fadhili zako wala kweli yakoKatika kusanyiko kubwa.

11. Nawe, BWANA, usinizuilie rehema zako,Fadhili zako na kweli yako na zinihifadhi daima.

Zab. 40