Zab. 39:7-11 Swahili Union Version (SUV)

7. Na sasa ninangoja nini, Ee Bwana?Matumaini yangu ni kwako.

8. Uniokoe na maasi yangu yote,Usinifanye laumu ya mpumbavu.

9. Nimenyamaza, sitafumbua kinywa changu,Maana Wewe ndiwe uliyeyafanya.

10. Uniondolee pigo lako;Kwa uadui wa mkono wako nimeangamia.

11. Ukimrudi mtu kwa kumkemea kwa uovu wake,Watowesha uzuri wake kama nondo.Kila mwanadamu ni ubatili.

Zab. 39