Zab. 37:8-12 Swahili Union Version (SUV)

8. Ukomeshe hasira, uache ghadhabu,Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya.

9. Maana watenda mabaya wataharibiwa,Bali wamngojao BWANA ndio watakaoirithi nchi.

10. Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo,Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo.

11. Bali wenye upole watairithi nchi,Watajifurahisha kwa wingi wa amani.

12. Asiye haki hunuia mabaya juu ya mwenye haki,Na kumsagia meno yake.

Zab. 37