6. Njia yao na iwe giza na utelezi,Malaika wa BWANA akiwafuatia.
7. Maana bila sababu wamenifichia wavu,Bila sababu wameichimbia shimo nafsi yangu.
8. Uharibifu na umpate kwa ghafula,Na wavu aliouficha umnase yeye mwenyewe;Kwa uharibifu aanguke ndani yake.
9. Na nafsi yangu itamfurahia BWANA,Na kuushangilia wokovu wake.