Zab. 27:10-13 Swahili Union Version (SUV)

10. Baba yangu na mama yangu wameniacha,Bali BWANA atanikaribisha kwake.

11. Ee BWANA, unifundishe njia yako,Na kuniongoza katika njia iliyonyoka;Kwa sababu yao wanaoniotea;

12. Usinitie katika nia ya watesi wangu;Maana mashahidi wa uongo wameniondokea,Nao watoao jeuri kama pumzi.

13. Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANAKatika nchi ya walio hai.

Zab. 27