Zab. 26:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. Ee BWANA, unihukumu mimi,Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu,Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi.

2. Ee BWANA, unijaribu na kunipima;Unisafishe mtima wangu na moyo wangu.

3. Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu,Nami nimekwenda katika kweli yako.

4. Sikuketi pamoja na watu wa ubatili,Wala sitaingia mnamo wanafiki.

Zab. 26