1. Ee BWANA, nakuinulia nafsi yangu,
2. Ee Mungu wangu,Nimekutumaini Wewe, nisiaibike,Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda.
3. Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja;Wataaibika watendao uhaini bila sababu.
4. Ee BWANA, unijulishe njia zako,Unifundishe mapito yako,
5. Uniongoze katika kweli yako,Na kunifundisha.Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu,Nakungoja Wewe mchana kutwa.