7. Inueni vichwa vyenu, enyi malango,Inukeni, enyi malango ya milele,Mfalme wa utukufu apate kuingia.
8. Ni nani Mfalme wa utukufu?BWANA mwenye nguvu, hodari,BWANA hodari wa vita.
9. Inueni vichwa vyenu, enyi malango,Naam, viinueni, enyi malango ya milele,Mfalme wa utukufu apate kuingia.