Zab. 22:6-12 Swahili Union Version (SUV)

6. Lakini mimi ni mdudu wala si mtu,Laumu ya wanadamu na mzaha wa watu.

7. Wote wanionao hunicheka sana,Hunifyonya, wakitikisa vichwa vyao;

8. Husema, Umtegemee BWANA; na amponye;Na amwokoe sasa, maana apendezwa naye.

9. Naam, Wewe ndiwe uliyenitoa tumboni,Ulinitumainisha matitini mwa mama yangu.

10. Kwako nalitupwa tangu tumboni,Toka tumboni mwa mamangu ndiwe Mungu wangu.

11. Usiwe mbali nami maana taabu i karibu,Kwa maana hakuna msaidizi.

12. Mafahali wengi wamenizunguka,Walio hodari wa Bashani wamenisonga;

Zab. 22