Zab. 22:14-18 Swahili Union Version (SUV)

14. Nimemwagika kama maji,Mifupa yangu yote imeteguka,Moyo wangu umekuwa kama nta,Na kuyeyuka ndani ya mtima wangu.

15. Nguvu zangu zimekauka kama gae,Ulimi wangu waambatana na taya zangu;Unaniweka katika mavumbi ya mauti

16. Kwa maana mbwa wamenizunguka;Kusanyiko la waovu wamenisonga;Wamenizua mikono na miguu.

17. Naweza kuihesabu mifupa yangu yote;Wao wananitazama na kunikodolea macho.

18. Wanagawanya nguo zangu,Na vazi langu wanalipigia kura.

Zab. 22