1. Mbona mataifa wanafanya ghasia,Na makabila wanatafakari ubatili?
2. Wafalme wa dunia wanajipanga,Na wakuu wanafanya shauri pamoja,Juu ya BWANA,Na juu ya masihi wake,
3. Na tuvipasue vifungo vyao,Na kuzitupia mbali nasi kamba zao.
4. Yeye aketiye mbinguni anacheka,Bwana anawafanyia dhihaka.