4. Sauti yao imeenea duniani mwote,Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.Katika hizo ameliwekea jua hema,
5. Kama bwana arusi akitoka chumbani mwake,Lafurahi kama mtu aliye hodariKwenda mbio katika njia yake.
6. Kutoka kwake lautoka mwisho wa mbingu,Na kuzunguka kwake hata miisho yake,Wala kwa hari yakeHakuna kitu kilichositirika.
7. Sheria ya BWANA ni kamilifu,Huiburudisha nafsi.Ushuhuda wa BWANA ni amini,Humtia mjinga hekima.
8. Maagizo ya BWANA ni ya adili,Huufurahisha moyo.Amri ya BWANA ni safi,Huyatia macho nuru.
9. Kicho cha BWANA ni kitakatifu,Kinadumu milele.Hukumu za BWANA ni kweli,Zina haki kabisa.