1. Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu,Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.
2. Mchana husemezana na mchana,Usiku hutolea usiku maarifa.
3. Hakuna lugha wala maneno,Sauti yao haisikilikani.
4. Sauti yao imeenea duniani mwote,Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.Katika hizo ameliwekea jua hema,
5. Kama bwana arusi akitoka chumbani mwake,Lafurahi kama mtu aliye hodariKwenda mbio katika njia yake.
6. Kutoka kwake lautoka mwisho wa mbingu,Na kuzunguka kwake hata miisho yake,Wala kwa hari yakeHakuna kitu kilichositirika.