Zab. 147:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. Haleluya.Msifuni Bwana;Maana ni vema kumwimbia Mungu wetu,Maana kwapendeza, kusifu ni kuzuri.

2. BWANA ndiye aijengaye Yerusalemu,Huwakusanya waliotawanyika wa Israeli.

3. Huwaponya waliopondeka moyo,Na kuziganga jeraha zao.

4. Huihesabu idadi ya nyota,Huzipa zote majina.

Zab. 147