1. Haleluya.Ee nafsi yangu, umsifu BWANA.
2. Nitamsifu BWANA muda ninaoishi,Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.
3. Msiwatumainie wakuu,Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.
4. Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake,Siku hiyo mawazo yake yapotea.
5. Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,Na tumaini lake ni kwa BWANA, Mungu wake,