Zab. 144:3-7 Swahili Union Version (SUV)

3. Ee BWANA, mtu ni kitu gani hata umjue?Na binadamu hata umwangalie?

4. Binadamu amefanana na ubatili,Siku zake ni kama kivuli kipitacho.

5. BWANA, uziinamishe mbingu zako, ushuke,Uiguse milima nayo itatoka moshi.

6. Utupe umeme, uwatawanye,Uipige mishale yako, uwafadhaishe.

7. Uinyoshe mikono yako toka juu, uniponye,Unitoe katika maji mengi, katika mkono wa wageni.

Zab. 144