Zab. 139:15-22 Swahili Union Version (SUV)

15. Mifupa yangu haikusitirika kwako,Nilipoumbwa kwa siri,Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi;

16. Macho yako yaliniona kabla sijakamilika;Chuoni mwako ziliandikwa zote pia,Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.

17. Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu;Jinsi ilivyo kubwa jumla yake!

18. Kama ningezihesabu ni nyingi kuliko mchanga;Niamkapo nikali pamoja nawe.

19. Ee Mungu, laiti ungewafisha waovu!Enyi watu wa damu, ondokeni kwangu;

20. Kwa maana wakuasi kwa ubaya,Adui zako wakutaja jina lako bure.

21. Je! BWANA nisiwachukie wanaokuchukia?Nisikirihike nao wakuasio?

22. Nawachukia kwa ukomo wa chuki,Wamekuwa adui kwangu.

Zab. 139