1. Nitakushukuru kwa moyo wangu wote,Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
2. Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu,Nitalishukuru jina lako,Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako,Kwa maana umeikuza ahadi yako,Kuliko jina lako lote.
3. Siku ile niliyokuita uliniitikia,Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
4. Ee BWANA, wafalme wote wa dunia watakushukuru,Watakapoyasikia maneno ya kinywa chako.