1. Haleluya.Lisifuni jina la BWANA,Enyi watumishi wa BWANA, sifuni.
2. Ninyi msimamao nyumbani mwa BWANA,Nyuani mwa nyumba ya Mungu wenu.
3. Msifuni BWANA kwa kuwa BWANA ni mwema,Liimbieni jina lake kwa maana lapendeza.
4. Kwa sababu BWANA amejichagulia Yakobo,Na Israeli, wawe watu wake hasa.
5. Maana najua mimi ya kuwa BWANA ni mkuu,Na Bwana wetu yu juu ya miungu yote.
6. BWANA amefanya kila lililompendeza,Katika mbingu na katika nchi,Katika bahari na katika vilindi vyote.