Zab. 13:2-5 Swahili Union Version (SUV)

2. Hata lini nifanye mashauri nafsini mwangu,Nikihuzunika moyoni mchana kutwa?Hata lini adui yangu atukuke juu yangu?

3. Ee BWANA, Mungu wangu, uangalie, uniitikie;Uyatie nuru macho yangu,Nisije nikalala usingizi wa mauti.

4. Adui yangu asije akasema, Nimemshinda;Watesi wangu wasifurahi ninapoondoshwa.

5. Nami nimezitumainia fadhili zako;Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.

Zab. 13