1. BWANA, uokoe, maana mcha Mungu amekoma,Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu.
2. Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe,Wenye midomo ya kujipendekeza;Husemezana kwa mioyo ya unafiki;
3. BWANA ataikata midomo yote ya kujipendekeza,Nao ulimi unenao maneno ya kiburi;