Zab. 119:88-101 Swahili Union Version (SUV)

88. Unihuishe kwa fadhili zako,Nami nitazishika shuhuda za kinywa chako.

89. Ee BWANA, neno lako lasimamaImara mbinguni hata milele.

90. Uaminifu wako upo kizazi baada ya kizazi,Umeiweka nchi, nayo inakaa.

91. Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo,Maana vitu vyote ni watumishi wako.

92. Kama sheria yako isingalikuwa furaha yangu,Hapo ningalipotea katika taabu zangu.

93. Hata milele sitayasahau maagizo yako,Maana kwa hayo umenihuisha.

94. Mimi ni wako, uniokoe,Kwa maana nimejifunza mausia yako.

95. Wasio haki wameniotea ili kunipoteza,Nitazitafakari shuhuda zako.

96. Nimeona ukamilifu wote kuwa na mwisho,Bali agizo lako ni pana mno.

97. Sheria yako naipenda mno ajabu,Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa.

98. Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu,Kwa maana ninayo sikuzote.

99. Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote,Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo.

100. Ninao ufahamu kuliko wazee,Kwa kuwa nimeyashika mausia yako.

101. Nimeiepusha miguu yangu na kila njia mbaya,Ili nilitii neno lako.

Zab. 119