66. Unifundishe akili na maarifa,Maana nimeyaamini maagizo yako.
67. Kabla sijateswa mimi nalipotea,Lakini sasa nimelitii neno lako.
68. Wewe U mwema na mtenda mema,Unifundishe amri zako.
69. Wenye kiburi wamenizulia uongo,Kwa moyo wangu wote nitayashika mausia yako.
70. Mioyo yao imenenepa kama shahamu,Mimi nimeifurahia sheria yako.