163. Nimeuchukia uongo, umenikirihi,Sheria yako nimeipenda.
164. Mara saba kila siku nakusifu,Kwa sababu ya hukumu za haki yako.
165. Wana amani nyingi waipendao sheria yako,Wala hawana la kuwakwaza.
166. Ee BWANA, nimeungojea wokovu wako,Na maagizo yako nimeyatenda.
167. Nafsi yangu imezishika shuhuda zako,Nami nazipenda mno.
168. Nimeyashika mausia yako na shuhuda zako,Maana njia zangu zote zi mbele zako.
169. Ee BWANA, kilio changu na kikukaribie,Unifahamishe sawasawa na neno lako.