Zab. 119:158-163 Swahili Union Version (SUV)

158. Nimewaona watendao uhaini nikachukizwa,Kwa sababu hawakulitii neno lako.

159. Uangalie niyapendavyo mausia yako,Ee BWANA, unihuishe sawasawa na fadhili zako.

160. Jumla ya neno lako ni kweli,Na kila hukumu ya haki yako ni ya milele.

161. Wakuu wameniudhi bure,Ila moyo wangu unayahofia maneno yako.

162. Naifurahia ahadi yako,Kama apataye mateka mengi.

163. Nimeuchukia uongo, umenikirihi,Sheria yako nimeipenda.

Zab. 119