141. Mimi ni mdogo, nadharauliwa,Lakini siyasahau mausia yako.
142. Haki yako ni haki ya milele,Na sheria yako ni kweli.
143. Taabu na dhiki zimenipata,Maagizo yako ni furaha yangu.
144. Haki ya shuhuda zako ni ya milele,Unifahamishe, nami nitaishi.
145. Nimeita kwa moyo wangu wote; Ee BWANA, uitike;Nitazishika amri zako.
146. Nimekuita Wewe, uniokoe,Nami nitazishika shuhuda zako.