106. Nimeapa nami nitaifikiliza,Kuzishika hukumu za haki yako.
107. Nimeteswa mno;Ee BWANA, unihuishe sawasawa na neno lako.
108. Ee BWANA, uziridhie sadaka za kinywa changu,Na kunifundisha hukumu zako.
109. Nafsi yangu imo mkononi mwangu daima,Lakini sheria yako sikuisahau.
110. Watendao uovu wamenitegea mtego,Lakini sikuikosa njia ya mausia yako.
111. Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele,Maana ndizo changamko la moyo wangu.
112. Nimeuelekeza moyo wangu nizitende amri zako,Daima, naam, hata milele.
113. Watu wa kusita-sita nawachukia,Lakini sheria yako naipenda.
114. Ndiwe sitara yangu na ngao yangu,Neno lako nimelingojea.
115. Enyi watenda mabaya, ondokeni kwangu,Niyashike maagizo ya Mungu wangu.
116. Unitegemeze sawasawa na ahadi yako, nikaishi,Wala usiniache niyaaibikie matumaini yangu.
117. Unisaidie nami nitakuwa salama,Nami nitaziangalia amri zako daima.