26. Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la BWANA;Tumewabarikia toka nyumbani mwa BWANA.
27. BWANA ndiye aliye Mungu,Naye ndiye aliyetupa nuru.Ifungeni dhabihu kwa kambaPembeni mwa madhabahu.
28. Ndiwe Mungu wangu, nami nitakushukuru,Ndiwe Mungu wangu, nami nitakutukuza.