Zab. 114:3-7 Swahili Union Version (SUV)

3. Bahari iliona ikakimbia,Yordani ilirudishwa nyuma.

4. Milima iliruka kama kondoo waume,Vilima kama wana-kondoo.

5. Ee bahari, una nini, ukimbie?Yordani, urudi nyuma?

6. Enyi milima, mruke kama kondoo waume?Enyi vilima, kama wana-kondoo?

7. Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana,Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo.

Zab. 114