Zab. 114:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Haleluya.Israeli alipotoka Misri,Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni.

2. Yuda ilikuwa patakatifu pake,Israeli milki yake.

3. Bahari iliona ikakimbia,Yordani ilirudishwa nyuma.

Zab. 114