Zab. 110:2-6 Swahili Union Version (SUV)

2. BWANA atainyosha toka SayuniFimbo ya nguvu zako.Uwe na enzi kati ya adui zako;

3. Watu wako wanajitoa kwa hiari,Siku ya uwezo wako;Kwa uzuri wa utakatifu,Tokea tumbo la asubuhi,Unao umande wa ujana wako.

4. BWANA ameapa,Wala hataghairi,Ndiwe kuhani hata milele,Kwa mfano wa Melkizedeki.

5. Bwana yu mkono wako wa kuume;Ataseta wafalme,Siku ya ghadhabu yake.

6. Atahukumu kati ya mataifa,Ataijaza nchi mizoga;Ataseta kichwa katika nchi nyingi.

Zab. 110