1. Ee Mungu, moyo wangu u thabiti,Nitaimba, nitaimba zaburi,Naam, kwa utukufu wangu.
2. Amka, kinanda na kinubi,Nitaamka alfajiri.
3. Ee BWANA, nitakushukuru kati ya watu,Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa.
4. Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni,Na uaminifu wako hata mawinguni.
5. Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.
6. Ili wapenzi wako waopolewe,Uokoe kwa mkono wako wa kuume, uniitikie.