Zab. 106:8-21 Swahili Union Version (SUV)

8. Lakini akawaokoa kwa ajili ya jina lake,Ayadhihirishe matendo yake makuu.

9. Akaikemea bahari ya Shamu ikakauka,Akawaongoza vilindini kana kwamba ni uwanda.

10. Akawaokoa na mkono wa mtu aliyewachukia,Na kuwakomboa na mkono wa adui zao.

11. Maji yakawafunika watesi wao,Hakusalia hata mmoja wao.

12. Ndipo walipoyaamini maneno yake,Waliziimba sifa zake.

13. Wakayasahau matendo yake kwa haraka,Hawakulingojea shauri lake.

14. Bali walitamani sana jangwani,Wakamjaribu Mungu nyikani.

15. Akawapa walichomtaka,Akawakondesha roho zao.

16. Wakamhusudu Musa matuoni,Na Haruni, mtakatifu wa BWANA.

17. Nchi ikapasuka ikammeza Dathani,Ikaufunika mkutano wa Abiramu.

18. Moto ukawaka katika mkutano wao,Miali yake ikawateketeza wabaya.

19. Walifanya ndama huko Horebu,Wakaisujudia sanamu ya kuyeyuka.

20. Wakaubadili utukufu waoKuwa mfano wa ng’ombe mla majani.

21. Wakamsahau Mungu, mwokozi wao,Aliyetenda makuu katika Misri.

Zab. 106