1. Haleluya.Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema,Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2. Nani awezaye kuyanena matendo makuu ya BWANA,Kuzihubiri sifa zake zote?
3. Heri washikao hukumu,Na kutenda haki sikuzote.
4. Ee BWANA, unikumbuke mimi,Kwa kibali uliyo nayo kwa watu wako.Unijilie kwa wokovu wako,