1. Haleluya.Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake,Wajulisheni watu matendo yake.
2. Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi,Zitafakarini ajabu zake zote.
3. Jisifuni kwa jina lake takatifu,Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA.
4. Mtakeni BWANA na nguvu zake,Utafuteni uso wake sikuzote.