22. Mungu, Mungu BWANA, naam, Mungu, Mungu BWANA, yeye yuajua, na Israeli naye atajua; kama ni katika uasi, au kama ni katika kosa juu ya BWANA, (usituokoe hivi leo);
23. sisi kujijengea madhabahu ili kukengeuka na kuacha kumwandama BWANA; au kama ni kusongeza juu yake sadaka ya kuteketezwa, au sadaka ya unga, au kama ni kusongeza sadaka za amani juu yake, yeye BWANA mwenyewe na alitake jambo hili;
24. au kama sisi tumefanya jambo hili kwa hadhari sana, tena makusudi, huku tukisema, Katika siku zijazo wana wenu yamkini wakanena na wana wetu, na kusema, Ninyi mna nini na BWANA, yeye Mungu wa Israeli?
25. Kwa kuwa yeye BWANA ameufanya huu mto wa Yordani uwe mpaka katikati ya sisi na ninyi, enyi wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, hamna fungu katika BWANA; basi hivyo wana wenu wangewakomesha wana wetu wasimche BWANA.