Yos. 19:2-10 Swahili Union Version (SUV)

2. Miji waliyokuwa nayo katika urithi wao ni Beer-sheba, na Sheba, na Molada;

3. na Hasarshuali, na Bala, na Esemu;

4. na Eltoladi, na Bethuli, na Horma;

5. na Siklagi, na Bethmarkabothi, na Hasarsusa;

6. na Bethlebaothi, na Sharuheni; miji kumi na mitatu, pamoja na vijiji vyake;

7. na Aini, na Rimoni, na Etheri, na Ashani; miji minne, pamoja na vijiji vyake;

8. tena vijiji vyote vilivyozunguka miji hiyo kote kote mpaka Baalath-beeri, Rama wa Kusini. Huo ndio urithi wa kabila ya wana wa Simeoni kwa kuandama jamaa zao.

9. Huo urithi wa hao wana wa Simeoni ulitoka katika fungu la wana wa Yuda; kwa maana hilo fungu la wana wa Yuda lilikuwa ni kubwa mno kwao; kwa hiyo wana wa Simeoni walikuwa na urithi katikati ya urithi wao.

10. Kisha kura ya tatu ilitokea kwa ajili ya wana wa Zabuloni kwa kuandama jamaa zao; na mpaka wa urithi wao ulifikilia hata Saridi;

Yos. 19