Yos. 19:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Kisha kura ya pili ilitokea kwa ajili ya Simeoni, maana, kwa ajili ya hiyo kabila ya wana wa Simeoni, kwa kuandama jamaa zao; na urithi wao ulikuwa katikati ya urithi wa wana wa Yuda.

2. Miji waliyokuwa nayo katika urithi wao ni Beer-sheba, na Sheba, na Molada;

3. na Hasarshuali, na Bala, na Esemu;

4. na Eltoladi, na Bethuli, na Horma;

5. na Siklagi, na Bethmarkabothi, na Hasarsusa;

6. na Bethlebaothi, na Sharuheni; miji kumi na mitatu, pamoja na vijiji vyake;

7. na Aini, na Rimoni, na Etheri, na Ashani; miji minne, pamoja na vijiji vyake;

8. tena vijiji vyote vilivyozunguka miji hiyo kote kote mpaka Baalath-beeri, Rama wa Kusini. Huo ndio urithi wa kabila ya wana wa Simeoni kwa kuandama jamaa zao.

9. Huo urithi wa hao wana wa Simeoni ulitoka katika fungu la wana wa Yuda; kwa maana hilo fungu la wana wa Yuda lilikuwa ni kubwa mno kwao; kwa hiyo wana wa Simeoni walikuwa na urithi katikati ya urithi wao.

Yos. 19