Yoe. 1:8-16 Swahili Union Version (SUV)

8. Ombolea kama mwanamwali avaaye maguniaKwa ajili ya mume wa ujana wake.

9. Sadaka ya unga na sadaka ya kinywajiZimekatiliwa mbali na nyumba ya BWANA;Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, wanaomboleza.

10. Shamba limeharibika, nchi inaomboleza; maana nafaka imeharibika, divai mpya imekauka, mafuta yamepunguka.

11. Tahayarini, enyi wakulima;Pigeni yowe, enyi watunzaji wa mizabibu;Kwa ajili ya ngano na shayiri,Maana mavuno ya mashamba yamepotea.

12. Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia;Nao mkomamanga na mtende na mtofaa;Naam, miti yote ya mashamba imekauka;Maana furaha imekauka katika wanadamu.

13. Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani;Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu;Njoni mlale usiku kucha katika magunia,Enyi wahudumu wa Mungu wangu;Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywajiZimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu.

14. Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini,Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi;Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu,Na kumlilia BWANA,

15. Ole wake siku hii!Kwa maana siku ya BWANA inakaribia, nayo itakuja kama uangamivu utokao kwake aliye Mwenyezi.

16. Je! Chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu? Naam, furaha na kicheko mbali na nyumba ya Mungu wetu?

Yoe. 1